MWANAMKE AAMTUPA MTOTO DILISHANI AKIWA NDANI YA BASI HUU NI UKATILI WA HALI YA JUU..

 Kamanda wa Polisi Singida, Thobias Sedoyeka amesema Jeshi la Polisi linamshikilia mwanamke
mmoja kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mjukuu wake ambapo alimtupa mtoto huyo kwenye dirisha la basi ambalo lilikuwa kasi, mwanamke huyo Waridi Saidi alimtupa mtoto huyo akiwa kwenye basi namba T 981 ALS  la kampuni ya  Salumu Classic lililotoka Dar kwenda Kigoma.
Mama huyo alimtupa mtoto huyo kijiji cha Iguguno, wilaya ya Mkalama alimtupa mjukuu wake Mayasa Meshaki, Dk  Adamu Hussein amesema  walimpokea mtoto akiwa katika hali mbay kutokana na kuvuja damu nyingi na siku ya pili alifariki  dunia  kutokana na jeraha la kupasuka kwa fuvu la kichwa.
Lawaridi amesema; dirisha lilikuwa wazi yani nilimshusha tu nikamchukua Mayasa nikamtupa bila kutegemea… Watu wakanivamia sasa huku wanapiga kelele kuanza kunipiga… Wamenipiga sana tu, basi gari ikasimama wakawa wameenda kumtafuta mtoto… nikaambiwa mtoto amepatikana lakini mpaka dakika hii sijamuona...

Popular posts from this blog