Timu 16 zilizofuzu kushiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015 huko Equatorial Guinea zimepangwa katika makundi manne usiku huu katika hafla ya upangaji makundi iliyofanyika jijini Malabo ambako fainali hizo zitafanyika .
Ligi kuu ya England imeendelea usiku huu kwa michezo mine iliyozikutanisha timu nane za ligi hiyo . Kwenye uwanja wa Emirates , Arsenal waliweza kushinda mchezo wao wa pili mfululizo baada ya kuwafunga Southampton 1-0 ukiwa ni ushindi wao wa pili mfululizo wakishinda kwa bao moja .