CHELSEA YAUA TATU DROGBA ATUPIA MMOJA......
Chelsea walishinda mchezo wao dhidi ya Tottenham kwa matokeo ya 3-0 .
Ushindi huo ulikuja baada ya mabao ya Edin Hazard , Didier Drogba na
Loic Remy . Katika mchezo mwingine Hull City na Everton walitoka sare ya 1-1 , na Man city wakawafunga Sunderland 1-4 .
Matokeo haya yanamaanisha kuwa Chelsea wanaendelea kuongoza ligi wakiwa na pointi 33 wakiwa wamewazidi Man city kwa pointi sita , Southampton ambao leo hii wamepoteza mchezo wao wa pili mfululizo wamejikuta wakishuka zaidi huku tofauti yao na Man United inayoshika nafasi ya 4 ikiwa pointi moja pekee .