KULA ZA WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI ZA FANYA MABADILIKO
Bunge la Afrika Mashariki limemfuta kazi aliyekuwa Spika wake Margaret Nantongo Zziwa
ambapo uamuzi huo umetokana na malalamiko ya kutumia vibaya ofisi yake kama Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).
Maamuzi hayo yamefikiwa leo katika makao makuu ya Bunge hilo Arusha,
ambapo Zziwa aliwahi kulalamikiwa na baadhi ya Wabunge kwamba anatumia
vibaya ofisi yake, amekuwa kitoa huduma isiyokidhi pamoja na ukosefu wa
heshima kwa Wabunge hivyo wawakilishi 45 kukubaliana kuhusu kufukuzwa
kwake kwa kupiga kura, ambapo jumla ya Wabunge waliokuwepo walikuwa 39,
kura za ndiyo zilikuwa 36 huku mbili zikisema hapana na nyingine moja
kuharibika.
Nilikurekodia sauti wakati habari hiyo ikiripotiwa na kituo cha WBS, unaweza kubonyeza play kuisikiliza.