USIYOYAJUA KUHUSU UAMISHO WA WELBECK........KUMBE MANCHESTER ILIMPA PESA ILIAONDOKE.......


BEKI wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand ameponda na kuhoji uamuzi wa timu hiyo kumpiga bei Danny Welbeck
hasa kwa wapinzani wao Arsenal.
Wakati Rio akishindwa kupata majibu, imefichuka kwamba United chini ya kocha wake mpya, Louis van Gaal, ilimlipa pesa Welbeck ili kukamilisha uhamisho wake wa kwenda Arsenal uliogharimu Pauni 16 milioni.
Welbeck, ambaye ametokea kwenye akademia ya klabu hiyo ya Old Trafford alipogundua analazimishwa kuhama aliomba alipwe pesa kitu ambacho United ilikifanya na kumlipa Pauni 1.5 milioni ili aende Arsenal.
Welbeck aliwekwa kwenye orodha ya wachezaji ambao hawakuwa kwenye mipango ya kocha Van Gaal kwenye klabu hiyo ya Old Trafford.
Hatimaye, straika huyo Mwingereza amekwenda kujiunga na Arsenal na kukabidhiwa jezi yenye Namba 23 atakayovaa na miamba hiyo ya Emirates.

Popular posts from this blog