Ndoa ya Wiz Khalifa na Amber Rose imefika ukingoni
Amber Rose anamshutumu Wiz Khalifa kuwa
amekuwa akimsaliti kwa kipindi kirefu na kumtolea sababu
zisizo na kichwa wala wa miguu
Vyanzo vilivyo karibu na Amber vimeiambia TMZ kuwa tangu kuanza kwa ziara ya Wiz
July mrembo huyo amekuwa akimhisi mume wake kuchepuka. Amber anawaambia
marafiki zake kuwa
alitaka kuungana na Wiz kwenye ziara hiyo lakini (Wiz) alikataa na
kumtaka akae nyumbani
kumwangalia mtoto wao
Anadai kuwa Wiz anataka kumtawala zaidi kwa kusema yeye ndiye
anatakiwa kutafuta mkate wa
kila siku na Amber akae tu nyumbani
Naye Wiz anadai kuwa ni Amber ndiye aliyemsaliti na Nick Cannon
Kupitia talaka hiyo, Amber anataka kuchukua udhibiti wa mtoto
wao Sebastian,mwenye umri
wa mwaka mmoja lakini atamruhusu Wiz kumtembelea mwanae.TMZ imedai
imeziona nyaraka
za talakaambazo
zinaonesha
kuwa wapenzi hao waliachana Jumatatu hii kwa kile kilichodaiwa tofauti
zisizosuluhishika