Haya hii ya leo ngoja niwatobolee siri kidogo tu kwenye upande wa mapenzi.
unajua
wanawake bwana tupo kama mayai ukiyaminya kidogo tu huwa yanapasuka..
sasa wengi wanaume huwa wanabaki kuropoa “wanawake hawaeleweki” WANATAKA
TUWEJE? Mwanamke huwa anapenda sana kuambiwa ukweli japo wengi wanadai
eti bila kudanganywa hatuingiliki, Wanawake wengi hupenda kuspend muda
wake zaidi na wake mpenzi
uliko na marafiki zake. Mwanamke hupenda
mwanaume anaejali zaidi kuliko mbabaishaji “sasa wewe jifanye gogo
tuone kama utapata mrembo” Jeuri ufanyiapo mwanamke dhahir huwa
unamvunja moyo na hukushusha thamani yako pindi umfanyiayo yakawa yale
yanayo mdharaulisha zaidi Mthamini mpenzi wako hata ukiwa na watu wengi,
onyesha unajali kuwa nae karibu, hujiona wa pekee Mwanamke hupenda
kusikilizwa japokuwa wanaume hujifanya vichwa na kutuona hatuna la
kuongea lakini sio kweli ni fikra zenu tu. Msikilize mpenzi wako uone
kama na wewe hatokusikiliza Mwanamke huthamini sana msg za mpenzi wake
kuliko simu apigiwayo na mwenza wake, maana kuona faraja zaidi pindi
asomapo msg hizo zaidi ya kupoteza muda kusubiri apigiwe au akupigie.
Msifie mkeo ama mchumba wako pindi apendezapo na kumpa faraja pindi
aumizwapo. Msikilize mchumba
wako na usitumie lugha ya ukali
akuombapo ushauri bali jaribu kuchunguza zaidi nini atakacho kwako. Kila
lililo dogo usilikuze bali lipe nafasi yake katika kutoa kipingamizi
ama makubaliano.lasivyo utasababisha kutokujiamini Onyesha unajali
Mkumbuke kila wakati hata mara 2 kwa siku Punguza jeuri na kauli chafu
ukifananya kati ya hayo hutopata misukosuko mingi na kumbuka kujishusha
endapo ufanyapo kosa na acha kutumia mabavu zaidi kuliko upole. haya
jamani ni hayo tu labda utaona umuhimu wa mwenza wako zaidi ya kuliko
kutoa lawama juu yake, wapendwa kama hamtojali kama kuna ambayo wakina
kaka nao wanatakaa kutoa kero zao uwanja wenu