UNYAMA MKUBWA AAMWAGIA MAJI YA MOTO MUMEWE
Mwanamke
mmoja katika wilaya ya Bunda, mkoani Mara, amemfanyia ukatili mume wake
kwa kumwagia maji ya moto yaliyokuwa yametengwa kwa ajili ya kupikia
ugali.
Kwa
mujibu wa jeshi la polisi wilayani hapa, tukio hilo lilitokea juzi, saa
4:30 usiku, katika mtaa wa Nyamakokoto, mjini Bunda, baada ya kuzuka
ugomvi ulitokana na mwanamke huyo (jina linahifadhiwa) kuchelewa kurudi
nyumbani.
Mwanaume
huyo amejeruhiwa vibaya mume wake sehemu mbalimbali za mwili wake, hali
iliyopelekea kulazwa katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Bunda.
Mwanaume huyo alisema sababu ya mke wake kummwagia maji ya moto ni kumuuliza sababu ya kuchelewa kurudi nyumbani kwani alirudi saa 4:30 usiku.
Mwanaume huyo alisema sababu ya mke wake kummwagia maji ya moto ni kumuuliza sababu ya kuchelewa kurudi nyumbani kwani alirudi saa 4:30 usiku.
Alisema
siku hiyo alitoka kazini kwake saa 1:00 usiku na kukuta mke wake ambaye
amezaa naye watoto wanne akiwa hajarejea nyumbani huku watoto
hawajetengewa chakula.
Alisema
baada ya kukuta hali hiyo aliamua kuchukuwa fedha na kwenda kununua
mboga ili aweze kuandaa chakula cha usiku akijua hawezi kurudi muda huo.
Alisema
baada ya kufika saa 4:00 usiku wakati watoto wake wameshabandika maji
ya kupikia ugali, aliamua kwenda kwa rafiki wa mke wake ili kuuliza
alipo mkewe, lakini walisema hawajamuona.
Alisema
aliamua kurejea nyumbani na ilipofika saa 4:30 usiku mwanamke huyo
alirejea na baada ya kumuuliza kwanini amechelewa kiasi hicho,
alichukuwa sufuria la maji ya moto na kumwagia.
Mganga
wa zamu katika hospitali ya Bunda, Dk. Bakari Ibrahimu, alisema
majeruhi huyo amejeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake, hasa
kifuani na mikononi na kwamba anaendelea na matibabu na hali yake
inaendelea vizuri.
Kwa
upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Philipo Kalangi,
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa mwanamke huyo
anashikiliwa na atafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya upelelezi
kukamilika.