UTATA MZITO KUHUSU ESCROW VIGOGO WATAJWA
ZITTO KABWE
Ripoti ya Kamati ya bunge ya Hesabu
za
Serikali imewataja baadhi ya vigogo wanaohusika na kashfa ya IPTL
Nchini Tanzania akiwemo Waziri Mkuu na kuwataka kuwajibika kisiasa na
kisheria.Sakata hiyo ya IPTL inahusihswa na upotevu wa mamilioni ya fedha na kwa muda mrefu umezusha mjadala mzito katika bunge la Tanzania.
Kamati hiyo imewataja viongozi wengine wanaotakiwa kuwajibika kutokana na kashfa hiyo kuwa ni mwanasheria,Waziri wa nishati na Madini, Naibu Waziri wa Nishati pamoja na viongozi wengine wa bodi.
Kashfa nyingine zilizowahi chukua uzito mkubwa katika bunge la Tanzania na kusababisha viongozi kuwajibika wakiwemo Waziri Mkuu ni pamoja na kashafa ya Richmond,EPA na sasa hii ya ESCROW ambayo kwa mara nyingine kamati hiyo imeonyesha wazi mapendekezo yake ya kutaka kuwajibika kwa waziri mkuu, Mawaziri na viongozi wengine.