jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linawasaka watu wasiofahamika wanaotuhumiwa
kuingia msikitini na kuiba jeneza, Wilaya ya Namtumbo, mkoani Ruvuma.Baada ya
kuiba jeneza hilo, watu hao wanadaiwa
kwenda nyumbani kwa Afisa wa Kijiji cha Kitanda, wilayani humo, Fidea Mbawala
na
kuliweka mlangoni, likiwa limesheheni matofali
Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Mihayo Msikhela, alisema tukio hilo lililotokea juzi,
saa 12:00 asubuhi, katika kijiji hicho
Alisema tukio hilo limesababisha kuwapo utata na kwamba uongozi wa
msikiti umedai kuwa tukio hilo ni la aina yake, ambalo halijawahi kutokea
Alisema tukio hilo liligundulika wakati waumini wa msikiti huo
walipokwenda kuswali swala ya alfajiri na kushtuka baada ya kusikia kuwa
jeneza hilo limekutwa kwenye mlango wa nyumba ya afisa mtendaji wa
kijiji hicho
Alisema kwa mujibu wa Katibu wa Msikiti huo, Khalifa Ngonyani, tukio hilo limezua
mtafaruku mkubwa kwa waumini wa msikiti huo
Kamanda Msikhela alisema taarifa za awali zinaonyesha kuwa tukio hilo
limefanyika baada ya afisa huyo kuwaeleza wananchi wa kijiji chicho kuwa
wanatakiwa kuchangia asilimia 75 ya ujenzi wa shule ya kutwa ya
sekondari ya Mkomanile
Alisema ujenzi wa shule hiyo ni utekelezaji wa agizo lililotolewa na
Rais Jakaya Kikwete na kwamba, wanakijiji waligoma kutoa michango hiyo
kwa madai kwamba, agizo hilo ni la ghafla na kuomba wachangie mwaka
2015, kwani kwa sasa nguvu zao wameelekeza kwenye kilimo
Msikhela alisema hakuna mtu aliyekamatwa na kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi