Kijana mmoja mwenye miaka 23 Jordan James Uingereza ameripotiwa kutumia paundi 100,000 za kimarekani sawa na zaidi ya milioni 160 za kitanzania ili afanyiwe upasuaji na kufanana kama mwanamitindo Kim Kadarshian.
Timu 16 zilizofuzu kushiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015 huko Equatorial Guinea zimepangwa katika makundi manne usiku huu katika hafla ya upangaji makundi iliyofanyika jijini Malabo ambako fainali hizo zitafanyika .
Ligi kuu ya England imeendelea usiku huu kwa michezo mine iliyozikutanisha timu nane za ligi hiyo . Kwenye uwanja wa Emirates , Arsenal waliweza kushinda mchezo wao wa pili mfululizo baada ya kuwafunga Southampton 1-0 ukiwa ni ushindi wao wa pili mfululizo wakishinda kwa bao moja .
Mwanamke mmoja katika wilaya ya Bunda, mkoani Mara, amemfanyia ukatili mume wake kwa kumwagia maji ya moto yaliyokuwa yametengwa kwa ajili ya kupikia ugali.
Mkuu wa kitengo cha kukabiliana na ubaguzi wa rangi katika shirikisho la soka duniani FIFA amesema kuwa ubaguzi wa rangi katika soka ya Uingereza unafanyika hadharani.
Watuamiaji wa simu za mkononi nchini Kenya,Rwanda na Uganda hivi karibuni watakuwa wakipiga simu kwa bei nafuu,baada ya wahudumu wa simu kukubaliana kupunguza ada ya kupiga simu katika eneo lolote la Afrika Mashariki.
Hatimaye Diamond Platnumz amefunguka kuhusu tetesi zinazoendelea kuwa ameachana na Wema Sepetu na kwamba ana mpango wa kufunga ndoa na Meninah Atick. Diamond ameiambia Bongo5 kuwa tetesi hizo zimekuwa zikimhuzunisha kwa kiasi kikubwa.